Kolonia Santita

Laana Ya Panthera Tigrisi

by Enock Maregesi


Formats

Softcover
$24.34
Hardcover
$41.19
Softcover
$24.34

Book Details

Language : Other
Publication Date : 9/17/2012

Format : Softcover
Dimensions : 6x9
Page Count : 406
ISBN : 9781477222959
Format : Hardcover
Dimensions : 6x9
Page Count : 406
ISBN : 9781477222966

About the Book

'Kolonia Santita: Laana Ya Panthera Tigrisi' ni hadithi ya kusisimua ya kijasusi na madawa ya kulevya iliyoandikwa na Enock Abiud Maregesi. Inazungumzia vita kati ya Tume ya Dunia ya Umoja wa Mataifa, ya kudhibiti madawa ya kulevya na ugaidi wa kimataifa, 'World Drugs Enforcement Commission' (WODEC) au Tume ya Dunia; na shirika kubwa la madawa ya kulevya la Kolonia Santita (CS-14) la Kolombia na Meksiko. Inaelezea, kwa kinagaubaga, jitihada za pamoja kati ya Tume ya Dunia, Marekani na Meksiko za kuwasaka na hatimaye kuwatia nguvuni viongozi nduli wa CS-14; na kuzuia shehena (kubwa) ya madawa ya kulevya na malighafi ya nyukilia: kwenda Afrika, Asia, Amerika, Ulaya – na kung’oa mizizi ya shirika la CS-14, lote, katika nchi za Hemisifi a ya Magharibi – na duniani kwa jumla.
Hiki ni kitabu cha kwanza cha aina yake cha kimataifa katika Tanzania. Lengo lake si tu kukata kiu ya wapenzi wa riwaya za kipelelezi na kufufua mwamko wa usomaji wa vitabu; ni kuleta, hali kadhalika, ufahamu na burudani ya kimataifa kwa Watanzania, Wakenya na Waganda – na jamii nzima ya Afrika ya Mashariki inayozungumza Kiswahili – na walowezi wa jamii yote ya Kiswahili duniani.


About the Author

Enock Abiud Maregesi alizaliwa Mwanza, Tanzania, na kukulia Musoma na Dar es Salaam, Novemba 25, 1972. Amesomea teknolojia ya habari na utawala wa biashara katika Chuo Kikuu cha Wales, na uandishi wa habari na vitabu katika chuo cha ubunifu wa kifasihi cha Manchester (The Writers Bureau) nchini Uingereza. Hadithi ya 'Kolonia Santita: Laana Ya Panthera Tigrisi' ni kitabu chake cha kwanza kilichohamasishwa na wakongwe wa riwaya wa Tanzania – kama Elvis Musiba, Euphrase Kezilahabi na Ben Mtobwa – na utafi ti yakinifu wa miaka kumi na nane wa ujasusi, madawa ya kulevya, ugaidi wa kimataifa na silaha za maangamizi za kikemia na kibiolojia. Anakaa Reading nchini Uingereza ambako anasoma na kufanya kazi.